CHAPATI ZA VIAZI / ALOO PARATHA 

Chapati za viazi ni chapati ambazo zinachanganywa na viazi mviringo vilivosagwa na kuchomwa kama chapati za kawaida, mikate hii asili yake ni kutoka ‘india’ inayojulikana kama ‘aloo paratha’ , ni mara yangu ya kwanza kuifanya so nimeamua kufanya simple recipe na matokeo yake nimeyapenda. 

MAHITAJI KWA CHAPATI

Unga wa ngano vikombe 2 

Samli vijiko 2 vya supu /ghee

Maziwa ya Unga kijiko 1 cha supu / milk powder  (sio lazima)

Chumvi kiasi 

Maji yabaridi 

MAHITAJI KWA VIAZI 

Viazi mviringo 3 vya kiasi 

Carrot 1 kubwa 

Chumvi 

Pilipili ya kuwasha kiasi

Bizari nyembamba / cumin powder 1 kijiko 1 cha chakula 

Pilipili manga kiasi /black pepper 

MATAYARISHO 

Menya viazi na carrot vikate kiasi, vikoshe na uvitie kwenye sufuria ,tia maji kiasi na chumvi, weka kwenye moto mpaka viwive vikauke maji

Vikishakauka maji epua tia pilipili manga,pilipili ya kuwasha na bizari nyembamba(uzile) , visage mpaka viwe havina madonge (viwe laini ) vionje chumvi kama ipo sawa weka pembeni. 

Chukua bakuli jengine changanya unga wa ngano, maziwa ya unga  (kama uko nayo) , chumvi na samli, mpaka uchanganyike, anza kutia maji kidogo kidogo mpaka donge lishikane, ukande unga uwe mlaini, 

Unga ugawe madonge kulinganga ukubwa wa chapati unazopenda, madonge 4 mpaka 6

Madonge utakayotoa, gawanya na viazi madonge sawa na ya unga 

Chukua donge 1 la unga lisukume kidogo juu yake weka donge 1 la viazi , lifunge donge la unga ndani yake mukiwa muna donge la viazi, weka pembeni 

Fanya hivyo mpaka unamaliza zote 

Weka pembeni japo dakika 10 hadi 30, anza kusukuma moja moja na uchome kwa moto wa kiasi 

Iweke chapati kwenye chuma/pan ikiwiva upande 1 igeuze upande wa pili, ukianza kuwiva upande wa pili tia mafuta au samli  kijiko 1 uzungushe kiasi wacha mpaka uwe rangi unayopenda , utoe na endelea na iliyobaki mpaka unamaliza. 

  • Kwenye viazi unaweza kuweka pilipili ya unga au nzima ukaikata kata, (nimetumia pilipili ya kupika pia naweza kuengeza viungo/spices unazopenda.

CAKE YA CHUNGWA /ORANGE CAKE

orangecake1

ORANGE CAKE (CAKE YA CHUNGWA)

Siagi ya kikopo nusu kg 500g

Sukari kikopo 1 (ulichotoa siagi )

Unga kikopo ulotoa siagi  viwili kasrobo (kimoja +nusu yake+robo yake )

Mayai 8 (medium )

Baking powder 1 tbsp

Chungwa 2 za kiasi (maganda na juice yake )

Washa oven 180 c au tayarisha mkaa wa moto  (wa kupambilia)

Saga siagi  na sukari  kwa muda wa dakika 5 mpaka 10 au mpaka uone imeshaanza kuwa nyeupe, anza kutia yai moja moja huku unasaga (hakikisha unasaga vizuri kabla kutia yai jengine ) , endelea na yai la pili usage mpaka unamaliza mayai,

ukimaliza kutia mayai na kusaga vizuri tia baking powder, changanya,

Chukua machungwa uyapare ngozi ya nje yote (tumia grater kupara ili itoke nyembamba na laini sana )

ipare ngozi ya orange yote na utie kwenye mchanganyiko wako na uchanganye vizuri, bakisha kidogo ya kuweka juu ya cake

Punguza speed ya machine yako  (mixer)

Yakate machungwa na ukamue yote kwenye mchanganyiko wako wa cake huku unatia unga kidogo kidogo,  mpaka unamaliza (unga na maji ya machungwa)

Chukua pan au sufuria weka baking paper chini (karatasi ya kupambilia ) ,weka mchanganyiko  na utandaze vizuri, na ubake kama kwa oven moto 180°c , kama kwa mkaa weka moto kiasi kwa muda wa dakika 45-55  inategemea na nguvu ya jiko lako,  ikishawiva iepue wacha ipoe itoe kwenye trey na cake ipo tayari kuliwa ni tam sana ladha na harufu utapenda.

  • Kabla ya kuepua ichome ujiti mpaka chini kuangalia kama imewiva (kama ujiti una maji maji basi cake haijawiva, kama ujiti mkavu cake imewiva.

NYAMA YA KONDOO YA VIUNGO / SPICY LAMB  

Kuna aina nyingi za upikaji wa nyama ya kondoo, moja ya njia rahisi na inayoleta ladha nzuri  ni kuikausha na viungo(spices) 

MAHITAJI 

Nyama ya kondoo kilo 1(iliyokatwa katwa)

Carrot 1 kubwa (iliyokatwakatwa)

Tomato 1 kubwa au 2 za kiasi (iliyokatwakatwa)

Kitunguu maji 1 (kilichokatwakatwa)

Pilipili za kijani 3 /green chillies 

Bizari nyembamba /cumin powder kijiko 1 cha supu 

Pilipili manga/black pepper  kijiko 1 cha chai 

Garam masala kijiko 1 cha supu 

Curry powder kijiko 1 cha supu 

Bizari ya mchuzi /tumeric powder kijiko 1 cha supu au nusu yake 

Pilipili ya kuwasha  

Chumvi 

Ndimu au limau 1

Kitunguu saum (garlic ) kijiko 1 cha supu

Tangawizi mbichi 

Mafuta ya kupikia /cooking oil vijiko 3 vya supu  (yakihitajika)

MATAYARISHO 

Ikoshe nyama itie kwenye sufuria pamoja na kitunguu saum, tangawizi na chumvi, iweke kwenye moto ichemke kwa dakika 3 hadi 5 , baada ya hapo itie maji kiasi ya kuwiva, funika ichemke, iwive na ikauke maji yote, 

Maji yakikauka kama nyama imetoa mafuta ni vizuri, kama haijatoa mafuta weka mafuta vijiko 3 vya supu, tia vitunguu maji , carrot na tomato, koroga uwache  dakika 2 hadi 3 tia spices zote, koroga  na funika ,wacha kwa dakika 5 hadi 7 kwa moto wa kiasi, 

Baada ya hapo kamulia ndimu au limau koroga kidogo epua na nyama ipo tayari kuliwa. 

  • Unaweza kuengeza au kupunguza viungo kulingana na unavyopenda. 
  • Pilipili ya kuwasha Nimeweka ya kupika  / unaweza kuweka ya unga au nzima .

SALAD YA MATUNDA / FRUITS SALAD 

MAHITAJI 

Ndizi mbivu 2

Papai 1

Strawberry 10 

Tikiti kiasi  (nimetumia tikiti manjano)

Embe mbivu 1 ya kiasi 

Sosi ya dessert  (nimetumia strawberry flavour dessert sauce ) 
Kosha, menya na ukate kate matunda kiasi unavyopenda, papai unaweza kulitoa kwa kujiko au kulikata kata kwa kisu pia, 

Weka kwenye combo chako na utie dessert sauce juu na ipo tayari kuliwa ikiwa kama ilivyo au unaweza kuiweka kwenye fridge kwa muda. 

Unaweza kuila tupu vile vile au unaweza ukatia maziwa ya maji.

  • Unaweza kupunguza matunda au kuengeza kulingana na unavyopenda .

UJI WA KUNDE 

MAHITAJI 

Kunde / red cow peas vikombe 2 (zichemshe ziwive zikauke)

Nazi/ tui vikombe 3-4

Pilipili manga (black pepper)kijiko 1 cha chai 

Iliki (cardamom) kijiko 1 cha chai 

Sukari (sugar)nusu kikombe au size unayopenda 

Unga wa ngano  (bread flour) kijiko 1 cha supu 

Karafuu kavu(dried cloves) chembe 2 (ukipenda)

Maziwa ya unga  (milk powder ) vijiko 2 vya supu  (ukipenda)

Chumvi  (salt) kidogo /pinch

KUNDE

MATAYARISHO

Kunde (zilizokwisha pikwa na kuwiva vizuri) zitie kwenye sufuria na vitu vyote pamoja isipokua unga wa ngano, 

Wacha zichemke kwa dakika 3 mpaka 5 , 

Pembeni koroga unga wa ngano na maji kidogo na utie kwenye uji wako unaochemka ili kuufanya uwe mzito, koroga kwa mda ili usifanye madonge mpaka ushikane, funika wacha uchemke mpaka uwe mzito kiasi unayopenda, epua na uji upo tayari. 

  • Unga wa ngano unaweza kukorogea maji au maziwa ya maji 
  • Kama uji wako unaweza kua mzito bila kuweka unga wa ngano, basi usiweke 
  • Unaweza kuengeza kiasi cha spices kulingana na unavyopenda .

CHAI YA MASALA/MASALA TEA

Chai ya masala ni chai ya viungo  (spices) ambayo unaweza kuipika vile unavyopenda, aidha ya maziwa au kavu, nikija upande wangu mimi napenda sana chai kavu, ila nikitamani chai ya maziwa lazima iwe ya masala , 

MAHITAJI 

Maziwa ya maji lita 1

Majani ya chai pakti 2 au vijiko 2 vya supu 

Zaatari kijiko 1 cha chai 

Iliki chembe 3

Karafuu kavu chembe 3

Mdalasini kipande 1 cha kiasi 

Tangawizi mbichi au kavu kiasi unachopenda 

Sukari 
Weka vitu vyote kwenye sufuria isipokua tangawizi na sukari  , unaweza kuengeza na maji au ukawacha maziwa matupu, 

Iweke kwenye moto wacha ichemke vizuri, 

Ikichemka vizuri kama imefanya mapovu juu ikoroge yale mapovu yaondoke, 

Hakikisha imeshachemka vizuri kwa dakika angalau 2 , saga tangawizi na utie kwenye chai, moto usiwe mdogo maziwa yanaweza kukatika , wacha ichemke tena kwa dakika 1 na epua , ichuje na Iweke/itie kwenye chupa au vikombe.

  • Unaweza kuweka sukari kabisa au unaweza kukorogea kwenye kikombe 
  • Ili maziwa yasikatike  hakikisha chai imechemka vizuri kabla kuweka tangawizi, AU yachemshe maziwa pekee kwanza mpaka yachemke vizuri ndio utie vitu viliobaki
  • Sufuria ya kupikia chai isiwe unapikia vyakula vyengine , bila hivo inaweza kusababisha chai/maziwa yakatike 
  • Ukipenda unaweza kutia mchaichai na pilipili manga, inazidi kua tamu.  

PILAU YA KUKU  (YA KUPIKA NA RICE COOKER)

Moja kati ya njia ninayoonaa ni rahisi na ya haraka kupika pilau ni kutumia rice cooker , leo nitaelezea jinsi ya kuipika na njia zinazofanya iwe rahisi zaidi.  

MAHITAJI 

Mchele nusu kg 

Kuku mlaini nusu kg

Viazi mviringo  (mbatata) 2 vimenye na vikate

Kitunguu saum  kijiko 1 cha supu (garlic)

Tangawizi mbichi kijiko 1 cha supu(ginger)

Bizari nyembamba  (uzile) kijiko 1 cha supu (cumin)

Mdalasini vipande 3 vya kiasi au kijiko 1 cha aupu(cinnamon)

Pilipili manga kijiko 1 cha chai (black pepper )

Kidonge cha supu cha kuku 1 (chicken maggi)

Garam masala kijiko 1 cha chai  (sio lazima)

Iliki chembe 4(cardamom)

Karafuu kava chembe 4(dried cloves)

Vitunguu maji kilichokaangwa kikombe 1 (nimetumia vitunguu maji vya kunnua, vipo tayari kupikia ) (onion)

Keroti  (carrot ) 1 , imenye na ikate ndogo ndogo 

Mafuta ya kupikia robo kikombe  (yakihitajika) (cooking oil)

Chumvi (salt)

Spaisi zote zikiwa za unga ni vizuri zaidi, 

Kwenye rice cooker, tia kuku uliekwisha mtengeneza na kumkosha vizuri ,chumvi, kitunguu saum, tangawizi, viazi , carrot, kidonge cha supu na spaisi zote 

Tia maji vikombe 3 au zaidi, inategemea na supu unayotaka kulingana na mchele wako, 

Funika ,washa rice cooker ,kuku achemke awive pamoja na viazi na ibaki na supu kiasi

Tia vitunguu maji , mchele na mafuta yakihitajika, kama kuku atakua na mafuta ya kutosha usitie mafuta, koroga kidogo funika wacha mpaka wali uwive ,ukauke ,funua uchanganye na pilau itakua tayari kuliwa.

●Kipimo cha supu inategemea na mchele utakaotumia au unaweza kutumia kipimo cha kikombe cha rice cooker, 

●Mara nyingi nakua nakisia maji au supu au nikitumia kipimo cha rice cooker naengeza kama kama nusu kikombe.

●unaweza kuengeza kiasi cha spaisi kama unataka pilau ikolee rangi.

●unapotumia kuku mlaini ndio unazidi kua rahisi sababu unatumia rice cooker kupikia na anawiva haraka. 

●unaweza kukaanga vitunguu mwenyewe vingi ukaweka kwenye fridge au freezer na kutumia unapovihitaji au unaweza kununua dukani vilivyokua tayari kutumia/vilivyokwisha kaangwa  (fried onions ).
VITUNGUU VILIVYOKWISHA KAANGWA

MUONEKANO WA VITUNGUU VYA KUNUNUA VILIVYOKAANGWA .

BAADHI YA HATUA UNAZOPITIA UNAPOPIKA PILAU KWENYE RICE COOKER 

PILAU YA SAMAKI WA KUKAANGA

​PILAU YA SAMAKI WA KUKAANGA

Tayarisha samaki wako wa kukaanga  kisha endelea na hatua nyengiene hapo chini. 

Mchele nusu kg

Viazi 2 (2 potatoes )

Kitunguu maji 1 kikubwa (onion)

Pilipili boga (capsicum ) kiasi. 

Bizari nyembamba 1 kijiko 1 change supu 

Pilipili manga kijiko 1 cha supu (black pepper)

Bay leaves 3

Mdalasini vipande 3 (cinnamon )

Iliki chembe 4 (cardamom )

Karafuu kavu chembe 4 (cloves )

Mafuta ya kupikia vijiko 5 vya supu

Kidonge cha supu 1 (maggi cube ) nimetumia vegetable maggi

Kitunguu saum kijiko 1 cha supu(garlic)

Tangawizi mbichi 1 kijiko 1 cha supu (ginger)
Roweka mchele kwa dakika 10 mpaka 30, 

Chukua bizari nzima, Pilipili manga, mdalasini, iliki, karafuu na bay leaves zipashe moto kwa sufuria au pan kwa dakika 2, kisha zisage zote kwa pamoja ziwe unga, 

Teleka sufuria kwenye moto weka mafuta, yakipata anza kukaanga viazi, vikikaribia kuwiva weka kitunguu maji, wacha kiwive kiasi weka pilipili boga , kitunguu saum na tangawizi, koroga kiasi wacha kwa dakika 1 au 2, tia kidonge cha supu pamoja na spices ulizozisaga, koroga  kidogo tu, weka maji yamoto kiasi ya kuwivisha wali , usiweke maji mengi, afadhali uweke kidogo badae ukiona hayajatosha uengeze, ukiongeza maji wakati ushaweka mchele lazima yawe yamoto bilateral hivyo  yanaweza kuharibu muonekano wa wali, )
Maji yakichemka angalia chumvi kama ipo sawa weka mchele koroga kidogo tu, punguza moto funika wacha uchemke kidogo kidogo mpaka unakauka, 

 funua koroga tena kidogo kuugeuza ukiona umeshawiva pambia au weka moto mdogo ,juu weka wale samaki uliowapika ili watie harufu wali na ufunike kwa dakika 15 mpaka 20 au mpaka uwive. 

Baada ya hapo funua mtoe samaki,  uchanganye taratibu bila kuuvuruga na pilau ipo tayari kuliwa 

 ANGALIZO; nimetumia mchele wa basmati. 

MIKATE YA KITUNGUU SAUM /SLESI ZA KITUNGUU SAUM

Moja kati ya pishi ambalo ni rahisi na halichukui muda mrefu kutayarisha na kupika ni slesi au mikate ya kitunguu saum  (garlic bread/garlic slices) 
MAHITAJI 
Mkate 1 (wowote)

Kitunguu saum kijiko 1 cha supu 

Siagi vijiko 3 hadi 5 vya supu 

Kotmiri kijiko 1 cha supu 
MATAYARISHO/KUPIKA 

Chukua mkate wako ukate kate slesi za kiasi, pia unaweza kukata mara 2 tu yaani unaugawa kati mara 2,weka pembeni, 

Chukua kibakuli changanya pamoja kitunguu saum kilichosagwa, siagi na kotmiri, 

Ipashe moto iyayuke vizuri, 

Ichanganye vizuri , kwa kutumia kijiko weka mchanganyiko wako kwenye kila slesi au upande mmoja wa mkate , 

Fanya hivyo mpaka unamaliza slesi zote, 

Washa oven, unaweza kutumia moto wa mkaa pia (sufuria na mkungu wa moto)

Hakikisha moto sio mkubwa , 

Weka slesi zako kwenye trey na uzichome/bake kwa moto wa juu na chini, ziwive ziwe light brown na crunchy, zitoe na zipo tayari kwa kuliwa, 

Ni tamu sana zinalika vizuri na chochote hata chai tu.

ZINGATIO; kotmiri unaweza kutumia freshi ukaisaga ila unapotumia ya unga inapendeza zaidi. 

      Unaweza kutayarisha slesi kiasi unachopenda na kuweka kwenye friza, na ukazichoma muda wowote unaopenda, sio lazima kuyayuka ukizitoa kwenye friza, unazichoma moja kwa moja. 

MCHANGANYIKO WA KITUNGUU SAUM, SIAGI NA KOTMIRI

 
SLESI ZA MKATE ZILIZOKATWA

 SLESI ZILIZOKWISHA PAKWA MCHANGANYIKO WA KITUNGUU SAUM 

 SLESI ZA KITUNGUU SAUM ZILIZOKWISHA KUCHOMWA/KUPAMBIWA TAYARI KWA KULIWA