WALI WA BIZARI / TUMERIC RICE

wp-image--1110608557Wali wa bizari ya mchuzi (tumeric powder) nimetumia recipe rahisi na hauna mahitaji mengi , nimeengeza vipande vya kidali cha kuku (chopped breast chicken) na  mchanganyiko wa mboga mboga ila unaweza ukawacha usiweke vitu hivyo kama utakua na kitoweyo chengine pembeni

MAHITAJI

Mchele nusu kg

Kidari cha kuku nusu kg

Mchanganyiko wa mboga mboga vikombe 2(kerot, mahindi machanga,maharage machanga,njegere)

Kitunguu maji 1

Tomato fresh 1

Kitunguu saum kijiko 1 cha chakula

Tangawizi mbichi kijiko 1 cha chakula

Bizari ya mchuzi kijiko 1 cha chai

Chumvi

Bizari nyembamba/ya pilau kijiko 1 cha chakula

Pilipili manga kiasi

Mafuta ya kupikia kiasi

MATAYARISHO

1.Kosha mchele roweka kwa dakika kadhaa , umwage maji, uchemshe mpaka uwive kiasi,mwaga maji uweke pembeni

2.Kataka kata kuku,kitunguu maji na tomato

3.Weka sufuria kwenye moto tia mafuta kiasi(vijiko 3 mpaka 5) , yakipata moto kaanga vitunguu maji ,dakika 2 Hadi 3 vilainike kiasi visiwe brown, tia vipande vya kuku, chumvi, kitunguu saum na tangawizi na bizari ya mchuzi, koroga, tia tomato pamoja na chumvi wacha mpaka viwive, (dakika 5)

4.tia mchanganyiko wa mboga mboga , bizari nyembamba,pilipili manga na koroga tena kidogo

5.Tia ule wali ulioupika koroga vizuri kuufanya uingirangi ya bizari wote, (pole pole bila kuuvuruga)

6.Weka moto mdogo mdogo funika kwa dakika 10 Hadi 15 au mpaka uwive na kukauka vizuri ,epua changanya vizuri na upo tayari kula na Enjoy .

  • Unaweza kuengeza rangi ya manjano mwishoni ukitaka ukolee rangi .

*sio lazima kutia kuku wala mboga mboga kama una kitooyo pembeni

3 thoughts on “WALI WA BIZARI / TUMERIC RICE”

Leave a comment